Mtafiti wa machozi Bergman anasema, "Kuzuia machozi huongeza viwango
vya shida, na huchangia magonjwa yaliyotokana na matatizo, kama
shinikizo la damu, matatizo ya moyo, na vidonda vya peptic.
MACHOZI
ni njia ya asili ya kuongea hisia za moja kwa moja kutoka moyoni lakini
pia
machozi ni njia ya kuongea vitu vingi kwa wakati mmoja.
TAFITI tofauti tofauti zilizofanyika zinaonyesha wanawake kati ya
asilimia 85 wanakiri kwamba baada ya kutoa machozi au kulia wanajisikia
ahueni, raha na wanakuwa 'relaxed'.
Kuna aina tatu za machozi ya binadamu
1. Emotional Tears: Haya ni machozi ambayo hutoka kutokana na kuguswa hisia, au kuumizwa moyoni.
2. Basal Tears: Haya ni machozi ambayo hufanya macho yetu kuwa na
majimaji kila wakati ( lubiricating tears) na kufanya macho yaone
vizuri.
3. Reflex Tears: Ni machozi ambayo huweza kutoka pale kitu kinachowasha
macho kuingia machoni kama vile kitunguu, mabomu ya machozi nk.
Faida za kutoa machozi
Machozi hutoa sumu: Hii ni kwa mujibu wa Biochemist William Frey,
ambaye ni mtafiti wa machozi anasema machozi huondoa sumu kutoka
mwilini.
Machozi huonesha uwazi na hutoa hisia za moyoni.
Kuondoa Stress; Wataalamu wanasema machozi yana kiwango kikubwa cha
madini ya Manganese na homoni za prolactin ambazo husaidia mliaji
kujisikia ahueni baada ya kumaliza kulia.
Kutoa machozi husaidia mwili kuondoa kemikali, Unapotoa machozi ukiwa
na hisia mwili huweza kutoa homoni za protein kama vile 'Leucine
Enkephalin', hupunguza stress zaidi na kukufanya ujisikie raha na
haueni.
Njia nzuri ya kulia au kutoa machozi,
Wataalamu wanashauri ukiona una stress, umekarisika ,umeumizwa ,una
mawazo au unajisikia kulia au kutoa machozi , tafuta sehemu ambayo ni
tulivu na ya siri (inaweza kuwa chumbani ukajifungia) peke yako, kisha
ruhusu kilio ambacho machozi yanayotiririka yenyewe hadi chini kwenye
mashavu, pia hakikisha unaruhusu hisia zako za ndani zihusike na kulia
kwako itakuwa ni tiba bora zaidi na utajisikia vizuri zaidi baada ya
kulia.
Angalizo
Usimzuie mtu kulia kama analia au anatoa machozi muache alie hadi
atosheke mwenyewe hiyo ndio dawa muhimu kwake ya kumfanya atoe kilicho
moyoni.
Muhimu
Inashauriwa mara baada ya kutoa machozi hakikisha unakuwa na mood nzuri,
mchangamfu kwani machozi pia husaidia 'ku-clear mind' (kusafisha
akili).
0 comments:
Post a Comment