IMANI haitegemei  matendo , bali matendo ni matokeo ya imani

Ukiweka kwa namna nyingine ni kwamba  tunachokiamni hakitokani na kile tunachofanya, bali tunafanya kutokana na kile tunachokiamini

Wokovu hautokani na matendo , bali hutokana na imani.

IMANI ILETAYO WOKOVU

  • Waefeso 2:8-9 “ kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani ambayo hiyo haijatokana na nafsi  zenu, ni kipawa cha Mungu , wala si kwa matendo mtu awaye yote asije akajisifu”

  • Neema ya Mungu iletayo wokovu huja kwa njia ya imani

  • Tunaposikia Neno la Mungu, mioyo yetu hufunguka  na imani huingia na kutujenga.

  • Hatuwezi kujidai katika imani kwa sababu Mungu ametupa tulipofungua mioyo yetu kusikia injili.

Warumi 4: 4-5 “ Lakini kwa mtu afanyaye kazi, ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni .Lakini kwa mtu asiyefanya kazi ,bali atamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki”

  • Kwa hiyo ili tupokee haki ni lazima tuwe na imani

  • Imani katika Yesu Kristo itokanayo na kusikia injili , hutolewa kwetu na Mungu mwenye haki. Waebrania 11: 6 “ maana pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu. Maana kila amwendeaye yeye ni lazima aamini kuwa yeye yupo, naye huwapa thawabu wale wamfuatao.”

  • Hakuna mwanadamu awezaye kumpendeza Mungu pasipo na Imani.

  • Hakuna mtu awezaye kumwendea Mungu pasipo imani

  • Hakuna mtu awezaye kupokea wokovu pasipo kuwa na imani itokanayo na kusikia neon la Mungu.


MFANO KATIKA BIBLIA

Kulikuwa na mtu jina lake ni Nikodemu aliyekuwa mtawala wa Wayahudi Nyakati za Yesu. Mtu alimwendea Yesu kwa siri usiku, akamuliza Yesu nifanye nini ili niweze kuurithi ufalme wa MUngu? Yesu akajibu na kusema (Yohana 3:3) “ Hakika hakika nakwambia mtu asipozaliwa mara ya pili  hawezi kuuona ufalme wa Mungu” Nikodemo alitaka kujua jinsi gani inavyowezekana kuzaliwa mara ya pili , akijua kwamba yeye ni mzee.

Yohana  3: 16-18 “ Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwana wake wa pekee ili kila mtu aaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma mwana ili ahukumu ulimwengu bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi , asiye amini amekwisha hukumiwa kwa sababu hakuliamini jina pekee la Mwana wa Mungu.” Warumi  10 :9-10

JE TUKIAMINI KITU GANI?

Tunahitaji kumwamini  Yesu ndani yetu ,aliye kufa kwa ajili ya dhambi zetu , alizikwa na siku ya tatu alifufuka katika wafu. Biblia inasema tukiamini na kukuiri kwa vinywa vyetu tutaokoka.

Mungu atatupa haki yake kwa neema. Sasa tutazaliwa mara ya pili kwa Roho Mtakatifu

IMANI INAWEZA KUTUMIKA WAPI?

  • Imani hutumika katika hali zote za maisha

  • Katika wokovu (Waefeso 2: 8) Galatia  3: 11

  • Kwenye maombi – 1Yohana 5: 14-15

  • Maeneo ya Uchumi na fedha – Wafilipi  4: 19

  • Kwenye chakula – Warumi  14 : 23

  • Kupata usingizi mtamu – Zaburi -127: 2; Zaburi  3 : 4-8

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Popular Posts