UBATIZO NI NI?
Ubatizo ni neno la Kigiriki ‘Baptizo’ lenye kumanisha :-
Kuchovya ( to dip)
Kuzamisha ( to submerge)
Kugharikisha( to overwhelm)
Kufunika kabisa kwa kimiminika
Kuchovya kitu katika kimiminika na kukitoa tena nje
HATUA ZA MKRISTO ILI KUBATIZWA UBATIZO WA MAJI MENGI
Toba : Matendo ya Mitume 2: 37 -38
Ni lazima toba ifanyike kabla ya kubatizwa ubatizo wa maji
mengi. Maana ubatizo ni ishara ya nje inayodhihirisha badiliko la ndani
lililofanyika katika moyo kupitia toba. Ubatizo pasipo badiliko la ndani na
mahusiano mapya na Mungu hauna tija.
Ni lazima kuamini : Mark
16: 15- 16 , Matendo 8: 36- 39
Ni pale tu tunapomwamini
Yesu Kristo mwana wa Mungu ndipo tubatizwe ubatizo wa maji mengi
.Tunaona Philipo na Towashi , ni pale tu Towashi alipomwamini Yesu ndipo
waliposhuka majini na kubatizwa , tazama Biblia inasema tena wakapanda kutoka
majini.
Ni lazima kuwa na ufahamu au nia njema ndani yako. 1Petro
3:21
Ni lazima kukubali kuwa mwanafunzi wa Yesu .Mathayo 28 : 19-
20 “Basi enendeni mkawafanye mataifa
yote kuwa wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba la Mwana na Roho
Mtakatifu, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi, na tazama mimi
nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari.”
FAIDA ZA KIROHO ZA UBATIZO WA MAJI MENGI
Kuelewa umuhimu wa kiroho
kubatizwa ubatizo wa maji
mengi soma Warumi 6: 3-7, Wakolosai 2: 12
0 comments:
Post a Comment