- Mungu
ametuamuru sisi tuwe na imani kwake, Marko 11: 22 "Yesu akajibu
akamwambia mwamini Mungu"
- Imani ni ya lazima
tunapomwendea Mungu na ili kumpendeza Mungu. Waebrania 11 : 6 "lakini
pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu , maana amwendeaye Mungu ni
lazima kuamini kwamba yupo , na kwamba yeye huwapa thawabu wale wamfuatao
- Kila tendo lisilo la IMANI ni
DHAMBI , Warumi 14 : 23 "Lakini aliye na shaka kama akila
amehukumiwa kuwa ana hatia , kwa maana hakula kwa imani . Na kila tendo
lisilotoka katika imani ni dhambi .”
- Imani hutusaidia kufikia NEEMA
ya Mungu , Warumi 5: 2 “ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani
kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake , na kufurahi katika
tumaini la utukufu wa Mungu.”
- Kwa imani tunashinda ulimwengu,
1Yohana 5: 4 “ Kwa maana kila
lkilichozaliwa na MUNGU huushinda ulimwengu na huku ndiko kuushindako
ulimwengu, hiyo imani yetu.”
- Ndiyo ngao ya Mkristo (Waefeso
6: 16) shika ngao ya imani
- Mwenye haki wangu ataishi kwa
imani ( 2 Wakoritho 5: 7) na Habakuki 2: 4.
TUNAIPATAJE IMANI ?
Ni kwa neon la Mungu tu Warumi 10: 17 “ Basi imani chanzo chake ni kusikia
na kusikia huja kwa neon la Kristo”
- Hili ni
andiko la msingi kwa kila aina ya imani
-
Imani ipo
mlangoni itasubiri iingie unaposikia nene la Mungu na kuliamini.
-
Imani huja
kwa njia mbalimbali ,imani huja kwa njia mbalimbali mojawapo ni :-
i. Kusoma
Biblia
ii. Kwa
kusikiliza mahubiri na shuhuda
iii. Kusoma vitabu
vizuri vya Kikristo
iv. Kutazama
filamu za Kikristo
v.
Kusikiliza
na kutazama video za Kikristo
Pia imani huja kwa kusikia neon la Mungu ,
neno la Mungu linaweza kuwa Logos- neno lililoandikwa toka kitabu cha mwanzo hadi ufunuo, Rhema – neon
lililosemwa.
i.
Linaweza
kuwa ni neon lililosemwa kwa sauti ndogo ya Roho mtakatif
ii.
Linaweza kuwa
Neno lililotoka kinywani toka madhabahuni
iii.
Linaweza kuwa
ni ushauri toka kwa wazazi, wazee au mtu yeyote anayekuzidi umri
iv.
Tusijifunge
kusikia neon na kuliamini hadi tusikie ‘Asema Bwana’
v. Ni lazima
kuwa makini ili kumsikia Roho Mtakatifu anaponena ndani yako au
kupitia mtu
mwingine.
0 comments:
Post a Comment