Je unajenga msingi wako juu ya kanisa au dhehebu lako?
Je unajenga kwa mtu? Mtume fulani au mhubiri fulani katika television au mchingaji fulani maarufu?
kwenye sherehe au taratibu fulani katika Kanisa?
1 Wakorintho 3: 11 "maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka , isipokuwa ni ule ulikwisha kuwekwa yaani Yesu Kristo . Katika kitabu cha Mathayo 16: 16-18 Petro anatambua Yesu kuwa ni Mwana wa Mungu aliyehai.Yesu akasema Petro juu yangu nitalijenga kanisa,Petro ni msingi wenyewe, jina Petro linatokana na neno la ARAMAIC,KEFAS lenye kumaanisha kipande cha jiwe au mawe madogo madogo(Pebbles). Pamoja na kwamba Petro alikuwa kiongozi wa Kanisa lakini yeye alikuwa si thabiti hata kanisa kujengwa juu yako.
Kuthibitisha haya soma maandiko yafuatayo: Mathay0 16:22;26:69-75: Galatia 2:11-14. Yesu ndiye mwamba hakuna mwamba mwingine, Isaya 28:16: Zaburi 18:2; 62:1-2,6-7; Matendo 4:11-12; Mathayo 7:21-27; Yohana 14:23-24
HITIMISHO.
Hakuna mtu awezaye kuweka msingi mwingine isipokuwa Yesu Kristo.
Msingi hauwezi kuwa Kanisa au dhehebu lako, Mtu au mtumishi fulani
BALI YESU KRISTO PEKE YAKE ALITESWA, KUFA KUZIKWA NA SIKU YA TATU ALIFUFUKA YU HAI HATA SASA.
0 comments:
Post a Comment