Paulo anawambia Warumi katika (Warumi 8: 18) kuwa "kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu" kwa hiyo mateso ambayo Mkristo unayapitia leo ni mepesi kulinganisha na utukufu utakaofunuliwa kwetu siku ya mwisho .

Mateso tunayopitia sasa ni ya kitambo kidogo tu. Tukivumilia hadi mwisho kuna utukufu mwingi wa milele utakaofunuliwa siku ya mwisho. Tukivumilia hadi mwisho kuna utukufu mwingi wa milele utakaofunuliwa siku ile ya

mwisho.

Biblia inasema katika kitabu cha Wakorintho ( 2 wakorintho 4: 17) "maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda tu , hutufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana"

MATESO YETU NI YA KITAMBO KIDOGO TU

Maandiko yafuatayo yanafafanua eneo hili:-

ZABURI  30 : 5 inasema " Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo katika radhi yake mna uhai . Huenda kilio huja kukaa usiku , lakini asubuhi huja furaha "  ISAYA  54 : 7-8 " Kwa kitambo kidogo nimekuacha , lakini kwa rehema nyingi nitakukusanya. Kwa ghadhabu ifurikayo nalikuficha uso wangu kwa kitambo , lakini kwa fadhili za milele nitakurehemu asema BWANA  mkombozi wako" YOHANA 16: 20 "amini amini nawambia, ninyi mtalia na kuomboleza, bali ulimwengu utafurahi, ninyi mtahuzunishwa lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha".

1 PETRO  1: 6 "mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo , ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali" 1PETRO 5: 10 " Na MUNGU wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika KRISTO , mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu" 

Inawezekana unapitia mateso kama mkristo na watu wengine wananong'ona kuwa mateso uliyonayo ni kutokana na dhambi. Usikate tamaa kwa kuwa BWANA hajakusahau wala kukuacha , kuna furaha inakuja asubuhi. Mungu atakuthibitisha na kukutia nguvu.

MATESO HUISHIA  KATIKA  FURAHA NA BARAKA

AYUBU 5: 17 "Tazama  yu heri mtu yule MUNGU amwadhibuye; kwa hiyo usidharau kurudiwa na huyo mwenyezi " Yakobo 5: 11 "Angalieni twaita heri waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake AYUBU, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma " ISAYA  61 : 2-3 " kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa na siku ya kisasi cha MUNGU wetu ; kuwafariji wote waliao. Kuwaagiza hao walio katika Sayuni wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la  sifa badala ya roho nzito, wapate kuitwa miti ya haki iliyopandwa na BWANA ili atukuzwe."

1Petro 4: 13 " Lakini kama mnavyoshiriki mateso ya Kristo, furahini ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe."

MATESO HUDHIHIRISHA UPENDO NA UAMINIFU WA MUNGU KWETU.

Kumbukumbu la Torati 8: 5 " Nawe fikiri moyoni mwako ya kuwa kama vile Baba amrudivyo mwanawe ndivyo BWANA MUNGU WAKO akurudivyo " ZABURI 119 : 75 "Najua kuwa hukumu zako ni za haki Ee Bwana, na kwa uaminifu umenitesa" Mithali 3: 12 " Kwa kuwa BWANA ampendaye humrudi, kama vile baba mwanaye ampendezaye"  WAKORINTHO 11: 32 " Ila tuhukumiwapo, twarudiwa na Bwana, isijeikatupasa adhabu pamoja na dunia" Ufunuo 3: 19 "Wote niwapendao mimi nawakemea na kuwarudi , basi uwe na bidii ukatubu."

HITIMISHO.

MUNGU awatendea kama wana, maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? " ZABURI 34 : 19 " Mateso ya mwenye haki ni mengi lakini BWANA humponya nayo yote."

Related Posts:

  • MATESO KWA MKRISTO NI LAZIMA YATIZAMIWE Katika kitabu cha (Yohana 16 : 33) Yesu alisema "Hayo nawambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki lakini jipeni moyo mimi nimeushinda ulimwengu. Pia katika kitabu cha (Matendo ya mitume 14: 22) Paulo … Read More
  • THE LAST DAYS OF JESUS JESUS  ENTERING  JERUSALEM On Palm Sunday  which is the Sunday before the Easter  Jesus  rode  from the Mount  of Olives  to Jerusalem  on  a Donkey. This happened … Read More
  • THE FAITH OF CANAANITE WOMAN Once when Jesus had gone into the region  of Sidon, a Canaanite woman from that area came to him and cried out "Have mercy  on me , O Lord , Son of David! my daughter is suffering from demon-possession " But Jes… Read More
  • THE MIRACLES OF JESUS -JESUS RAISES THE SON OF A WIDOW When  Jesus came to a small  town called  Nain, a dead man who was the only son of a widow, was being carried  out to be burried. A large crowd from the town was there with her. When Jesus  saw her … Read More
  • UBATIZO NA FAIDA ZAKE Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE MicrosoftInternetExplorer4 … Read More

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Popular Posts