Katika kitabu cha (Yohana 16 : 33) Yesu alisema "Hayo nawambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki lakini jipeni moyo mimi nimeushinda ulimwengu. Pia katika kitabu cha (Matendo ya mitume 14: 22) Paulo anasema "wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile imani, nayakwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya
dhiki nyingi".
Maandiko hapo juu yanaonyesha wazi kuwa wakristo ni lazima wategemee dhiki. Tukichunguza kwa undani maandiko haya yanaonyesha :-
Kama mkristo wajibu wako kujua kwamba upitapo katika dhiki au mateso unatakiwa uwe na amani badala ya hofu.
Ni lazima tujipe moyo tupitapo katika dhiki/mateso au majaribu, na hii nikwasababu Yesu ameushinda ulimwengu.
Yeye(Yesu) alishinda maumivu, mateso na kifo na baadaye alifufuka toka katika wafu
0 comments:
Post a Comment