Taarifa kutoka Momba mkoani Songwe
zinaeleza kwamba askari polisi wa kitengo cha usalama barabarani mwanaume
ambaye jina lake halijawekwa wazi mwenye umri wa miaka 29 anadaiwa
kumuua mpenzi wake kwa kumchinja na kitu chenye
ncha kali.
Tukio hilo kusikitisha limetokea
jana Jumamosi Januari 6,2018 asubuhi jirani kabisa na kituo cha polisi Kamsamba
kilichopo tarafa ya Kamsamba wilaya ya Momba mkoani Songwe ambapo askari huyo
alikwenda kutekeleza unyama huo kwa mpenzi wake Winfrida Bedwin Lucas ambaye ni
muuguzi katika kituo cha afya cha Kamsamba .
Baada ya ofisa huyo wa polisi
kutimiza haja yake inasemekana kwamba alikuwa kazini katika kituo hicho cha
Kamsamba na alikwenda katika ghala la silaha na kuchukua bunduki kisha kujipiga
risasi ya shingo na maisha yake yakaishia hapo hapo.
Mtoa taarifa wetu anaeleza kwamba
chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi ambapo askari polisi alikuwa
akimtuhumu mpenzi wake huyo (nesi) kutokuwa mwaminifu na kuwa na mahusiano na
wanaume wengine.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema
kuwa askari huyo alikuwa anamtaka kwa nguvu kumuoa mwanamke huyo.
"Winfrida alikuwa nesi katika
kituo cha Afya kamsamba,ameuwawa kwa kuchinjwa kama kuku na askari polisi-kituo
cha polisi Kamsamba, alikuwa anamtaka kwa nguvu kumuoa na kukataliwa,akaenda
akaanua nguo za binti na akampigia simu aende akachukue nguo zake
alipofika pale jamaa akamkamata akampiga kisu na yeye kwenda ofisini akachukua
bunduki akajiua",kimeeleza chanzo chetu kingine cha habari.
Mwili wa marehemu unatarajiwa
kuzikwa kesho Jumatatu mkoani Mbeya.
0 comments:
Post a Comment