WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema kuwa, ofisi yake haiungi mkono mfumo wa kazi kwa mikataba.

Waziri Mkuchika ameongeza kuwa, mfumo huo ni gharama kubwa ukilinganisha na kuajiri mfanyakazi kwa ajira ya kudumu na kwamba wizara yake inashughulikia suala hilo na kwamba hivi karibuni taasisi za umma hazitaruhusiwa kuajiri wafanyakazi wapya kwa mfumo wa mikataba.

“Tunataka kila ofisi kuajiri kwa mujibu wa mahitaji, hatutaruhusu mfumo huu wa mikataba kuendelea kwa sababu ni gharama kubwa mno kwa serikali,” alisema.


Kuhusu wafanyakazi wanaokwenda likizo maalum,  waziri alisema yeyote atakayekwenda katika likizo ya namna hiyo atatakiwa kuwasilisha nyaraka zake wizarani lini anarudi na wale watakaowasilisha barua kuwa wamerudi wanatakiwa kusubiri jibu la serikali.

“Kama ulikuwa nje ya nchi au ofisi mfano miaka mitano, ni dhahiri kuna mtu alijaza nafasi yako, hivyo unaporudi, unatakiwa kuwasilisha barua na kuipa nafasi serikali kujibu,” alifafanua Waziri Mkuchika.

Ameeleza kwamba, suala la likizo  maalum sio jambo jipya katika mfumo wa utumishi wa umma na umekuwa ukitumika katika nchi nyingi duniani

“Hatuna shida nayo, lakini tunataka wafuate taratibu sahihi wanaporudi.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuchika amesema kuwa, Bodi ya Mishahara na Maslahi (HSRB) iko katika hatua za mwisho za kurekebisha mfumo mzima wa mishahara, utakaondoa tofauti ya uwiano wa mishahara katika taasisi za umma kwa wafanyakazi wenye ujuzi, sifa na uzoefu.

Related Posts:

  • The Demand for a Sign MATHEW 16:1-4 (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({}); The Pharisees also with the Sadducees came, and tempting desired him that he would show them a sign from heaven. He answered and said unto them, When it… Read More
  • The Birth of John the Baptist LUKE 1:57-66  Now Elisabeth’s full time came that she should be delivered ; and she brought forth a son. And her neighbors and her cousins heard how the Lord had showed great mercy upon her ; and they rejoiced with … Read More
  • The Feeding of the Four Thousand MATHEW 15:32-39¶ Then Jesus called his disciples unto him, and said, I have compassion on the multitude, because they continue with me now three days, and have nothing to eat : and I will not send them away fasting, lest the… Read More
  • Mary Visits Elisabeth  LUKE 1:39-56 (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({});  And Mary arose in those days, and went into the hill country with haste, into a city of Judah ; and entered into the house of Zechariah, and… Read More
  • The Feeding of the Five Thousand   MATHEW  14:13-21 When Jesus heard of it, he departed thence by ship into a desert place apart : and when the people had heard thereof, they followed him on foot out of the cities. And Jesus went forth, and saw a… Read More

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Popular Posts