Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi ametangaza na kutoa agizo kwa
viongozi wa Halmshauri ya Kinondoni kuanza kutoa mikopo ya vitendea
kazi kwa vijana mbalimbali wilayani huo zikiwemo Pikipiki ili vijana
waweze kujikwamua kiuchumi.
Ali Hapi amesema hayo alipowatembelea Wafanyabiashara wa soko la
ndizi ambao wanategemewa kuhamishwa katika eneo la Kigogo Dampo siku za
karibuni na kudai kuwa zipo fedha zaidi ya Bilioni 1 kwa ajili ya mikopo
kwa vikundi vya vijana na kina mama ambazo zimekuwa hazitoki kwa kuwa
watu wamekuwa hawataki kijiunga katika vikundi na kwenda kukopa.
"Vijana wanaotaka kukopa Pikipiki waje, waje
wajiorodheshe wakopeshwe Pikipiki walete rejesho serikalini tuna
Billioni 1 imekaa tuu pale eti tunasubiri vijana waje, watakuja lini?
Sasa nataka kuona vijana wananufaika na fedha hizo wajikwamue ili
familia zao nazo zinufaike" Alisema Hapi
Mkuu wa Wilaya aliendelea kusisitiza kuwa "Nataka
tuwakopeshe watu vitu ambavyo vinawasaidia moja kwa moja, tunataka
tuwakopeshe watu dhana za kufanyia kazi nimeshaanza kumwambia Mkurugenzi
jambo hilo walifanye. Naibu Meya wakijitokeza vijana 400 Kinondoni
tukawakopesha Pikipiki nataka nikuakikishie ndani ya muda mfupi fedha
zile zinarudi, mpe mtu Pikipiki chukua kadi itunze yeye analeta
marejesho kila wiki unauhakika hapo"
0 comments:
Post a Comment