Wamesamehewa na kuokolewa, wakati mtu anapoona ya kwamba amemuasi  Mungu mara elfu na ya kwamba dhambi zake zinamwelekeza  jehanamu.Anapoona ya kwamba Kristo amempenda na ameichukua adhabu ya dhambi hizo zote na ya kwamba zimesamehewa na kusahaulika, je, hataweza  kufurahi? je mwanamaji anapookolewa toka kwa kaburi ya maji  hafurahi?

 Msomaji- haungalikuwa na furaha  kuu  zaidi ukijua ya kwamba dhambi zako zimesamehewa? Kwa sasa huthubutu kuwaza juu ya kifo au juu  ya hukumu au juu ya jehanamu.Wakati Roho wa Mungu anapoyaleta mambo haya katika mawazo yako, unajaribu kuyafutia mbali.Biblia inasema "Heri mtu yule ambaye dhambi zake zimesamehewa ambaye dhambi zake zimefunikwa".

Mungu anawapenda wakristo nao wanampenda. Ni raha kiasi gani kwa mkristo kujua  kwamba anaye  Yesu, rafiki huyu mpendwa aliye naye kila siku kila saa, kumwongoza na kumhifadhi na kumtimizia mahitaji yake yote.Mtume Petro alisema kumhusu Yesu "Naye mwampenda ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa  hamwoni sasa mnamwamini na kufurahi sana kwa furaha isiyoonekana , yeye utukufu."

"Wakristo wana ushirika na Mungu - kuzungumza na Mungu na Mungu kuzungumza nao. Ni furaha iliyoje Mkristo anapoifungua Biblia na kusema " Nena Bwana mtumishi wako anasikia." Na je ni furaha kuu  iliopo  wakati mwingine katika umati mkuu, ukimtukuza na kumhimidi Baba yetu wa mbinguni, au kuketi mezani mwa mwanamke kwa furaha kuu.

Wakristo wana furaha  kwa kushinda  dhambi, kwa kumpenda Mungu, na kwa kuwafanyia wema watu wengine.

Biblia inasema Kwa kuzitii amri za Mungu kuna tunzo kuu, Mkristo anapofanya mambo hayo kumpendeza Yesu Kristo mwokozi wake ni fuaraha ya kiasi gani wanayotoa!

Related Posts:

  • Who is God? (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({ google_ad_client: "ca-pub-3375027849950266", enable_page_level_ads: true }); window.dataLayer = window.dataLayer || []; function gtag(){dataLayer.push… Read More
  • Why Should I Read the Bible? (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({}); (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({ google_ad_client: "ca-pub-3375027849950266", enable_page_level_ads: true }); window.dataLayer… Read More
  • Who is Jesus? (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({ google_ad_client: "ca-pub-3375027849950266", enable_page_level_ads: true }); window.dataLayer = window.dataLayer || []; function gtag(){dataLayer.push(… Read More
  • Help Someone Find God window.dataLayer = window.dataLayer || []; function gtag(){dataLayer.push(arguments);} gtag('js', new Date()); gtag('config', 'UA-109612802-1'); (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({ google_… Read More
  • How can you be sure that you have accepted Christ? (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({ google_ad_client: "ca-pub-3375027849950266", enable_page_level_ads: true }); window.dataLayer = window.dataLayer || []; function gtag(){dataLayer.push… Read More

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive

Popular Posts