Neno mkristo limetumika mara tatu katika agano jipya (Matendo 11:26;
Matendo 26:28; Petero WA kwanza 4:16). Wafuasi wa yesu kristo waliitwa
kwa mara ya kwanza “wakristo” antiokia (Matendo 11:26) kwa sababu tabia
zao, matendo yao na hotuba zao zilikuwa kama za Kristo. Ilitumika
kiasili na watu wasiookoka wa Antiokia kama jina la kimajazi kuwadhihaki
wakristo hao. Ina maana sawa na “Kuwa mmoja wa kundi la kristo” au
“mfuasi wa kristo,” ambayo imefanana na tafsiri ya Neno hili katika
kamusi ya Webster.
Kwa bahati mbaya, neno mkristo limepoteza kwa kiwango kikubwa usawa wa
matumizi yake na Linatumika mara kwa mara kumaanisha tu mtu mwenye dini
au pengine muadilifu kinyume cha Mfuasi halisi wa yesu kristo
aliyezaliwa mara ya pili. Watu wengi wasioamini na kuwa na tumaini ndani
ya yesu kristo hujichukulia tu kuwa ni wakristo kwa sababu wanahudhuria
ibada za kanisa ama wanaishi katika taifa la kikristo. Lakini, kuenda
kanisani, kuwahudumia wale wasiobahatika maishani au kuwa mtu mzuri
haviwezi kukufanya kuwa mkristo. Kama muinjilisti mmoja alivyosema,
“kuenda kanisani hakufanyi mtu kuwa mkristo sawa na mtu kuenda gereji
hakumfanyi kuwa gari.” Kuwa mshirika wa kanisa anayehudhuria ibada kila
mara na kutoa kwa ajili ya kazi za kanisa hakuwezi kukufanya wewe kuwa
mkristo.
Biblia inatufundisha ya kwamba matendo yetu mema tunayoyatenda hayawezi
kutufanya tukubalike mbele za Mwenyezi Mungu. Tito 3:5 inatuambia ya
kwamba “si kwa matendo ya haki tuliyoyatenda, ila kwa huruma zake
alituokoa kwa kutuosha na kutufanya upya kwa roho Mtakatifu.” Kwa hivyo
mkristo nimtu aliyezaliwa mara ya pili na Mungu (Yohana 3:3; Yohana 3:7;
Petero wa kwanza 1:23) na aliyeweka imani na tumaini lake lote ndani ya
yesu kristo. Waefeso 2:8 inatuambia ya kwamba “Kwa neema mmeokolewa
kupitia imani wala si kwa ajili yenu wenyewe bali ni kipawa cha Mungu.”
Mkristo wa kweli ni mtu aliyetubu dhambi zake na kuweka imani na tumaini
lake ndani ya Yesu kristo pekee. Imani yao haimo ndani ya kufuata dini
ama kanuni Fulani za uadilifu ama miongozo ya kusema fanya hiki na
usifanye kile.
Mkristo wa kweli ni mtu aliyeweka imani na tumaini lake lote ndani ya
utu wa Yesu kristo na kukubali ya kwamba alikufa msalabani kwa fidia ya
dhambi zetu na akafufuka tena siku ya tatu kupata ushindi dhidi ya kifo
ili awape uzima wa milele wote wamwaminio. Yohana 1:12 inatuambia ya
kwamba “wote waliomwamini aliwapa uwezo kuwa wana wa mungu, kwa wale
waliaminio jina lake.” Mkristo wa kweli ni mwana wa Mungu halisi, sehemu
ya jamii halisi ya mungu na aliyepewa maisha mapya ndani ya kristo.
Alama ya mkristo wa kweli ni upendo kwa wengine na utiifu kwa neno la
Mungu (Yohana wa kwanza 2:4; Yohana wa kwanza 2:10).
Related Posts:
JE UNAJENGA KATIKA MSINGI UPI?
Je unajenga msingi wako juu ya kanisa au dhehebu lako?
Je unajenga kwa mtu? Mtume fulani au mhubiri fulani katika television au mchingaji fulani maarufu?
kwenye sherehe au taratibu fulani katika Kanisa?
1 Wakor… Read More
IMANI NA MATENDO, JE TUKIAMINI KITU GANI?
Normal
0
false
false
false
EN-US
X-NONE
X-NONE
MicrosoftInternetExplorer4
… Read More
Providing For Our NeedsSo do not worry, saying, 'What shall we eat?' or 'What shall we drink?' or
'What shall we wear?' For the pagans run after all these things, and your
heavenly Father knows that you need them. But seek first His k… Read More
MATESO KWA MKRISTO NI MEPESI
Paulo anawambia Warumi katika (Warumi 8: 18) kuwa "kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu ule utakaofunuliwa kwetu" kwa hiyo mateso ambayo Mkristo unayapitia leo ni mepesi kulinganisha na… Read More
Blessings From God"But
blessed is the man who trusts in the LORD, whose confidence is in him.
He will be like a tree planted by the water that sends out its roots by
the stream. It does not fear when heat comes; its leaves are a… Read More
0 comments:
Post a Comment